Hali ya huzuni ilitanda katika kijiji cha Silibwet eneo la Nessuit, kaunti ndogo ya Njoro, kaunti ya Nakuru, baada ya dada wawili kusombwa na mafuriko walipojaribu kuvuka mto Ndaruga.
Akithibitisha kisa hicho, chifu wa eneo hilo Douglas Mutai, alisema shughuli za kuwatafuta zinaendelea kwa usaidizi wa wapiga mbizi wa eneo hilo.
Wasichana hao wawili Sharon Chepngetitch na Faith Cheptoo ni wanafunzi wa shule ya msingi ya Tegitech, katika gredi ya sita na saba mtawalia.
Wakazi wa eneo hilo sasa wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Nakuru kujenga daraja katika sehemu hiyo.