Home Habari Kuu Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa na Polisi Nairobi

Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa na Polisi Nairobi

0

Washukiwa wawili wa mauaji waliokuwa wakisakwa na polisi, wamekamatwa na maafisa wa upelelezi wa maswala ya jinai, DCI, Jijini Nairobi.

Wawili hao Nehemia Odhiambo almaarufu Oti na Emmanuel Otieno almaarufu Emasu, walikamatwa katika maficho yao mtaani Baraka na Dandora mtawalia.

Washukiwa hao wanadaiwa kumdunga kisu mtu mmoja alfajiri ya  tarehe saba mwezi Machi mwaka huu, kabla ya kwenda mafichoni.

Kulingana na uchunguzi wa polisi, watatu hao walikuwa wakitembea pamoja kabla ya kutofautiana. Mmoja wa washukiwa hao alichomoa kisu na kundunga mwenzake kifuani. Alifariki akipokea matibabu katika kituo kimoja cha afya.

Polisi wamewahusisha washukiwa hao na misururu ya visa vya uhalifu katika mitaa ya Baba dogo, Huruma na Lucky Summer.

Website | + posts