Home Vipindi Washukiwa watatu wa wizi wa kebo watiwa nguvuni Emali

Washukiwa watatu wa wizi wa kebo watiwa nguvuni Emali

Kebo hizo, mali ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom, zilipatikana zikisafirishwa kwa gari aina ya Probox, katika eneo la Kyumbi.

0
kra

Maafisa wa upelelezi wamewatia mbaroni washukiwa watatu na kunasa shehena ya Kebo za deta, zinazoaminika kuibwa katika eneo la Emali, Kaunti ya Makueni.

Wakati wa oparesheni iliyofanywa na maafisa hao, Kebo hizo, mali ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom, zilipatikana zikisafirishwa kwa gari aina ya Probox, katika eneo la Kyumbi, kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.

kra

Oparesheni hiyo ilifanywa kufwatia ripoti iliyoandikishwa katika kituo cha polisi cha Emali na bawabu aliyefichua wizi huo.

Washukiwa Cosmas Mutuku, Dominic Bosire na Mulwa Nguthu, wanazuiliwa na polisi ili wafikishwe mahakamani  siku ya Jumatatu kujibu mashtaka dhidi yao.

Website | + posts