Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa, wamewakamata washukiwa watano wanaoaminika kuwa wanachama wa genge ambalo limekuwa likiwahangaisha wakazi wa eneo la Sargoi na viunga vyake.
Washukiwa hao ambao ni Vincent Ochieng, Shadrack Ochieng, Felix Otieno, Salim Ali na Shafi Yusuf, awali walinaswa katika kanda ya video, wakionyesha mali waliyoiba kutoka kwa waathiriwa.
Baada ya upekuzi, maafisa wa polisi walipata koti la samawati lililoonekana katika video hiyo, simu tatu aina ya iphones, simu aina ya samsung na simu aina ya memojo miongoni mwa vifaa vingine.
Kulingana na idara ya upelelezi wa jinai, DCI, watano hao wanazuiliwa na polisi huku wakisubiri kufikishwa mahakamani.