Washukiwa watano wa Al Shabaab wauawa Garisa

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa watano wa kundi la wanamgambi wa al Shabaab wameuawa Jumamamosi eneo la Fafi kaunti ya Garissa .

Kulingana na taarifa za polisi washukiwa wengine wanne walikamatwa .

Polisi walifanya shambulizi la kushtukia wakati wanamgambo hao walikuwa wakivuka mpaka kuingia nchini ili kuweka kambi eneo la Fafi.

Bunduki mbili aina ya PKM machine guns, moja ya RPM, sita za AK47 na vilipuzi kadhaa zilipatikana.

Waliokamatwa wanachunguzwa zaidi na polisi ili kubaini nia ya kundi hilo.

Website |  + posts
Share This Article