Home Kaunti Washukiwa wanne mahakamani kwa kughushi vyeti vya masomo

Washukiwa wanne mahakamani kwa kughushi vyeti vya masomo

Washukiwa wanne wamefikishwa mahakamani mjini Eldoret kwa tuhuma za kughushi vyeti vya masomo katika harakati za kusaka ajira.

Bethwel Kipkoech, Celestine Cherop Chepsoi, Eddah Cheptanui Boit na Jackson Kipkogei walikanusha madai hayo na wakaachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu shilingi 100,000 au bondi ya shilingi 300,000.

Walishtakiwa kwa makosa ya kughushi vyeti vya taaluma, kutengeneza nyaraka za uongo, kutoa nyaraka za uongo na kujipatia mali ya umma kwa njia ya udanganyifu.

Wanne hao wanatuhumiwa kwa kughushi stakabadhi kwa minajili kupata kazi za utumishi wa umma katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi.

Website | + posts
Alphas Lagat
+ posts