Home Kaunti Washukiwa wa wizi wakamatwa Mombasa

Washukiwa wa wizi wakamatwa Mombasa

Washukiwa hao wanazuiliwa, huku polisi wakiendeleza uchunguzi.

0
kra

Washukiwa wawili wanaohusishwa na visa vya wizi mjini Mombasa, wamekamatwa na maafisa wa polisi wa idara ya kukabilana na makosa ya jinai DCI.

Wawili hao Mohammed Ibrahim Shaban mwenye umri wa miaka 22 na Abdulaziz Ali Ogutu mwenye umri wa miaka 19, walikamatwa walipokuwa katika maficho yao katika kijiji cha Utange, walikokuwa wakipanga shambulizi lingine la wizi.

kra

Washukiwa hao ambao hutumia panga na pikipiki, wanahusishwa na misururu ya uhalifu ambayo imewahangaisha wakazi wa Mombasa, ikiwa ni pamoja na kisa kilichonakiliwa Julai 18,2024.

Kulingana na maafisa wa DCI, washukiwa hao pia wanahusishwa na visa tofauti vilivyoropotiwa Septemba 14, 2024, katika maeneo ya Majengo, Makupa na Tononoka.

Wakati wa kuwakamata washukiwa hao, maafisa wa polisi walinasa vifaa kadhaa ikiwa ni pamoja na panga, visu vitatu, simu mbili za rununu na kitambulisho cha taifa kinachomilikiwa na Yusuf Amani Yusuf.

Washukiwa hao wanazuiliwa, huku polisi wakiendeleza uchunguzi.

Website | + posts