Home Kaunti Washukiwa wa wizi wa vifaa vya elektroniki wakamatwa Kisii

Washukiwa wa wizi wa vifaa vya elektroniki wakamatwa Kisii

Bidhaa hizo zilizonaswa, zilijumuisha simu za rununu 351, vipakatalishi 33 na vifaa vingine 21 vya kielektroniki.

0
Vifaa vya wizi vyanaswa Kisii.

Maafisa wa huduma ya taifa ya polisi wameimarisha vita dhidi ya vifaa vya kielektoniki katika kaunti ya Kisii.

Mnamo siku ya Jumatano, maafisa wa polisi kutoka kaunti ndogo ya Kisii ya kati, walinasa bidhaa za elekroniki zinazoshukiwa ziliibwa kutoka kwa wananchi.

Bidhaa hizo zilizonaswa, zilijumuisha simu za rununu 351, vipakatalishi 33 na vifaa vingine 21 vya kielektroniki.

Katika operesheni iliyofanywa na maafisa hao mjini Kisii, washukiwa 14 wa wizi za vifaa vya kielektroniki pia walikamatwa na wanazuiliwa na polisi.

Hayo yanajiri siku chache baada ya maafisa wa polisi Jijini Nairobi, kuwanasa washukiwa wanne wa wizi wa simu.

Maafisa wa polisi wa kitengo cha DCI, waliwanasa Malumasi Aisha na Agaba Anestus ambao ni raia wa taifa moja jirani, pamoja na  Sarah Njeri dadake Mary Wangui raia wa Kenya, baada ya operesheni iliyotekelezwa kati kati ya Jiji la Nairobi.

Idara ya DCI ilisema imefunga mianya yote ya biashara ya simu za wizi hapa nchini.