Home Kimataifa Washukiwa wa wizi wa shilingi milioni 2.2 wakamatwa

Washukiwa wa wizi wa shilingi milioni 2.2 wakamatwa

0
kra

Washukiwa sita wakiwemo maafisa wanne wa polisi wanaoaminika kumfuata kabla ya kuvunja gari la mhasibu wa Shule ya Kimataifa ya Rophine, na kutoweka na shilingi milioni 2.2 wamekamatwa.

Kulingana na maafisa wa DCI, washukiwa hao walimfuata mhasibu huyo kutoka benki moja huko utawala, ambapo alikuwa ametoa pesa zilizokusudiwa kulipa wafanyikazi wa shule ya Rophine. Wasita hao walikamatwa katika uwanja wa maegesho ya umma, katika Kituo cha Polisi cha Kasarani.

kra

Walipopekuliwa, shilingi 350,000 zilipatikana kwenye gari walilokuwa wakitumia huku shilingi 123,000 zikitolewa mifukoni mwao. Pesa hizo zinaaminika kuwa sehemu ya shilingi milioni 2.2 zilizoibwa. Mkuu wa DCI katika eneo hilo alithibitisha kuwa maafisa waliokamatwa hawakuwa kazini rasmi huko Utawala wala hawakutekeleza kazi chini ya maagizo yake.

Washukiwa hao wamewekwa chini ya ulinzi mkali huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Jemie Saburi
+ posts