Home Michezo Washukiwa wa mauaji ya mwanariadha wa Uganda wakamatwa

Washukiwa wa mauaji ya mwanariadha wa Uganda wakamatwa

0

Polisi mjini Eldoret wamewakamata washukiwa wawili wakuu wa mauaji ya mwanariadha wa Uganda Benjamin Kiplagat.

Kiplagat aliye na umri wa miaka 37, alipatikana akiwa amefariki kwenye gari siku ya Jumapili akiwa na majeraha ya kisu.

Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Moiben Stephen Okal, amethibitisha kukamatwa kwa washukiwa hao akiwemo mwendeshaji boda boda huku pia wakipatikana na kisu kilichotumika kwa mauji hayo.

Mwanariadha huyo akiyekuwa akiishi Elgeyo Marakwet, aliiwakilisha Uganda katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016.

Website | + posts