Makala ya tano ya mashindano ya Kip Keino Classic Continental Tour yatakayoandaliwa tarehe 20 mwezi huu katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, yamewavutia washindi wa medali za Olimpiki katika mbio na michezo ya uwanjani.
Katibu katika Wizara ya Michezo Peter Tum, aliyehudhuria hafla ya uzinduzi uwanjani Nyayo siku ya Alhamisi,alikariri kujitolea kwa serikali kufanikisha mashindano hayo.
“Mashindano haya ni muhimu kwa wizara ya michezo na ndio maana tutaendelea kuunga mkono mashindano kama haya.Tutaendelea kuunga mkono Kip Keino Classic kwa njia kubwa,” akasema katibu
Kwa upande wake kinara wa chama cha riadha nchini Jackson Tuwei amefichua mipango ya kutuma maombi kuandaa mashindano ya Diamond League, na endapo watafaulu ,yatakuwa mashindano ya pili ya Diamond League kufanyika barani Afrika baada ya mkondo wa Rabat.
“Tunamtaka kila mmoja kujitokeza kutazama mashindano hayo,tumetuma maombi ya kuandaa mashindano ya Diamond League na pia mashindano ya Diamond League na yale ya dunia mwaka 2029 .”akasema Tuwei.
Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir amewarai Wakenya kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa mashindano hayo .
Mashindano ya Kenya yatakuwa ya pili katika msururu wa makala 11 ya continental tour ya kiwango cha dhahabu na yatashuhudia bingwa mtetezi wa mita 100 Ferdinad Omanyala akizindua uhasama dhidi ya Keneth Bednarek wa Marekanmi.
Itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo kurejea uwanjani Nyayo tangu mwaka 2020 wakati wa Covid 19.
Benki ya ABSA imefadhili mashindano hayo kwa kima cha shilingi milioni 40 .
Mkurugenzi wa mauzo wa benki ya Absa Moses Muthui amesema wataendelea kuwekeza katika mashindano hayo.
“Absa inaamini katika kuwekeza kwa wanaspoti wa Kenya .Kwa miaka kumi iliyopita tumewekeza zaidi ya shilingi bilioni 1 .2 kwa michezo nchini Kenya ikiwemo riadha,gofu na soka na tutaendelea kuunga mkono michezo nchini.”akasema Muthui.”akasema Muthui