Home Kaunti Washindi wa mashindano ya riadha ya Kapsabet watuzwa

Washindi wa mashindano ya riadha ya Kapsabet watuzwa

0

Marion Kibor na Amos Kiplagat ni miongoni mwa wanariadha 40 waliotuzwa mjini Kapsabet katika Kaunti ya mabingwa ya Nandi, baada ya kushiriki na kushinda mashindano ya mbio za Kapsabet Half Marathon yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.

Kibor kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet anasema baada ya kushiriki mbio hizo za kilomita 21, sasa anaendelea kufanya mazoezi kambini kwa bidii ili aweze kushiriki mbio za Amsterdam mwezi wa Oktoba.

Hata hivyo, washikadau mbalimbali Katika sekta ya michezo na ya utalii waliodhamini mbio hizo za Kapsabet Half Marathon wanasema ipo aja kwa wanariadha chipukizi kutuzwa na kuandaliwa mazingira kabambe ili kupata motisha ya kukuza na kuboresha talanta zao.

Washindi walionyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za kilomita 21 na 10 kwa wasichana na wavulana mtawalia wamepokezwa kitita cha shilingi 250,000 kila mmoja.

Website | + posts
Kimutai Murisha
+ posts