Washindi wa medali za dhahabu ,fedha na shaba katika raga ya wachezaji saba upande wanaume katika michezo ya Olimpiki jijini Paris,Ufaransa watabainika kesho.
Katika mechi za nusu fainali Afrika Kusini itakumbana na wenyeji Ufaransa, huku mabingwa watetezi Fiji wakipimana nguvu na Australia.
Argentina itachuana na New Zealand kuwania nafasi za 7-8 nao Ireland wakwangurane na Marekani.
Kenya itashuka uwanjani dhidi ya Samoa katika mchuano wa kuwania nafasi ya 9-10,yakiwa maruduo baada ya Samoa kuikomoa Kenya 26-0 katika kundi B.