Home Kimataifa Waokoaji wa Morocco wawatafuta manusura kwa kuchimba kwa mikono

Waokoaji wa Morocco wawatafuta manusura kwa kuchimba kwa mikono

0

Katika vijiji vya mbali vya milimani kusini mwa Marrakesh, waokoaji wanapambana kutafuta manusura baada ya tetemeko kuu la ardhi lililotokea Ijumaa usiku.

Wamekuwa wakitumia mikono kuwatafuta manusura huku mamlaka ikihangaika kutuma vifaa kwenye barabara zilizojaa vifusi, na vijiji vingine vikiwa magofu.

Idadi rasmi ya vifo ni zaidi ya 2,100, lakini kumekuwa na tahadhari kuwa idadi inaweza kuongezeka kadiri ukubwa wa uharibifu unavyozidi.

Wafanyakazi wa dharura kutoka nje ya Morocco sasa wamejiunga na juhudi za uokoaji, usaidizi unaohitajika sana, kwani kila saa inayopita inapunguza uwezekano wa kupata manusura.

Rabat imekubali misaada kutoka Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ufaransa, Marekani na baadhi ya nchi nyingine wanasema wako tayari kusaidia. Uhispania imetuma waokoaji 86 katika timu mbili, na mbwa wanne wa kunusa.

BBC
+ posts