Mshindi wa nishani ya fedha ya Dunia Emmanuel Wanyonyi na bingwa mara mbili wa Jumuiya ya Madola Wycliff Kinyamal watashiriki nusu fainali ya mita 800 Ijumaa katika michezo ya Olimpiki.
Kinyamal atashiriki mchujo wa pili wa nusu fainali kuanzia saa sita unusu adhuhuri leo Ijumaa huku Wanyonyi akishiriki mchujo wa tatu.
Fainali ya mbio hizo itaandaliwa kesho usiku.
Kenya italenga kuhifadhi taji hiyo ambayo imetwaa tangu mwaka 2008 jijini Beijing nchini China.