Home Michezo Wanyonyi ateuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha chipukizi bora wa mwaka

Wanyonyi ateuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha chipukizi bora wa mwaka

Wanyonyi ametamba msimu huu akiibuka mshindi wa mbio za nyika duniani katika mbio za kupokezakana kijiti   mseto,kabla ya kushinda mikondo mitatau ya Diamond League ,mashindano ya Rabat,Paris na Xiamen.

0
EUGENE, OREGON - JULY 23: Emmanuel Wanyonyi of Team Kenya competes in the Men's 800m Final on day nine of the World Athletics Championships Oregon22 at Hayward Field on July 23, 2022 in Eugene, Oregon. (Photo by Carmen Mandato/Getty Images)

Mshindi wa  nishani ya fedha dunia  mwaka huu katika mbio za mita 800,Emmanuel Wanyonyi, ameteuliwa katika orodha ya mwisho ya wanariadha watatu wanaowania tuzo ya chipukizi bora wa mwaka ya shirikisho la Riadha Ulimwenguni.

Wanyonyi ametamba msimu huu akiibuka mshindi wa mbio za nyika duniani katika shindano la kupokezakana kijiti   mseto,kabla ya kushinda mikondo mitatau ya Diamond League ,mashindano ya Rabat,Paris na Xiamen.

Wengine wanaowania tuzo hiyo ni Roshawn Clarke wa Jamaica, aliyemaliza wa nne katika mita 400 kuruka viunzi  wakati wa mashindano ya dunia na  Erriyon Knighton wa Marekani  aliyeshinda medali ya fedha ya dunia katika mita 200.

Mshindi atatangazwa tarehe 11 mwezi ujao kwenye hafla itakayoandaliwa mjini Monaco Ufaransa.

Website | + posts