Home Kimataifa Wanyonyi anusia rekodi ya Dunia huku Moraa akitamba Lausane

Wanyonyi anusia rekodi ya Dunia huku Moraa akitamba Lausane

0

Bingwa wa Olimpiki Emmanuel Wanyonyi alisajili muda wa pili wa kasi ulimwenguni wa mbio za mita 800 katika mashindano ya Diamond League ya Laussane Alhamisi usiku huku bingwa wa Dunia Mary Moraa akishinda pia mbio za vipusa.

Wanyonyi aliziparakasa mbio hizo kwa dakika 1 sekunde 41.11, ukiwa muda wa pili wa kasi baada ya Rekodi ya Dunia ya dakika 1 sekunde 40.91 inayoshikiliwa na David Rudisha.

Moraa ambaye pia ni mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki  alitwaa ushindi kwa dakika 1 sekunde 57.91.

Mary Moraa akishindaLa mbio za mita 800 katika mashindano ya Lausane Diamond League

Reynold Cheruiyot na Brian Komen walimaliza katika nafasi za 5 an 6 katika mita 1,500 zilizoshindwa na bingwa wa Dunia Yakub Ingebrigsten wa Norway kwa muda wa dakika 3 sekunde 27.83.

Katika mita 3,000 wanawake, Janeth Chepng’etich wa Kenya alimaliza wa pili akisajili muda wa dakika 8 sekunde 23.48.

Deribe Welteji wa Ethiopia alitwaa nafasi ya kwanza kwa dakika 8 sekunde 21.50.

Bingwa wa Olimpiki Letsile Tebogo aliendeleza ubabe wake katika mita 200 akirekodi muda wa kasi wa sekunde 19.64.

Website | + posts