Emmanuel Wanyonyi ndiye bingwa mpya wa Olimpiki wa mita 800 baada ya kuparakasa fainali kwa dakika 1 sekunde 41.19.
Marco Arop wa Canada ameshinda fedha kwa dakika 1 sekunde 41.20, huku shaba ikitwaliwa na Djamel Sedjati wa Algeria.
Ushindi wa Wanyonyi aliye na umri wa miaka 20 ameendeleza ubabe wa Kenya katika mbio za mita 800, kwenye mashindano ya Olimpiki kwa mara ya tano mtawalia tangu mwaka 2008.
Wilfred Bungei alishinda dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008 kabla ya David Rudisha kutawazwa bingwa mwaka 2012 na kuhifadhi tena mwaka 2016.
Emmanuel Korir alishinda medali ya dhahabu mwaka 2021 mjini Tokyo.