Home Habari Kuu Wanjiku Wakogi ateuliwa mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya naibu Rais

Wanjiku Wakogi ateuliwa mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya naibu Rais

Wakogi anachukua mahala pa George McGoye, ambaye mwezi Oktoba aliteuliwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Djibouti.

0

Wanjiku Wakogi ndiye mkuu mpya wa wafanyakazi katika afisi ya naibu Rais Rigathi Gachagua.

Wakogi anachukua mahala pa George McGoye, ambaye mwezi Oktoba aliteuliwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Djibouti.

Kupitia kwa taarifa, Gachagua alisema Wakogi ni mtumishi wa umma aliye na uzoefu wa muda mrefu, ambaye amehudumu katika afisi na idara mbali mbali za serikali.

Wakogi amepanda ngazi serikalini, na amehudumu wadhifa wa katibu katika kamati ya serikali ya kutoa ushauri ushauri.

“Uteuzi huo wake unaleta nguvu mpya katika utekelezaji wa majukumu katika afisi ya naibu Rais. Tutamuunga mkono kikamilifu anapoongoza kundi la wafanyakazi,” alisema Gachagua.

Aidha naibu huyo wa Rais alimpongeza McGoye kwa kujitolea mhanga alipofanya kazi Katika afisi ya naibu Rais.

“Tunamshukuru kwa uongozi mwema anapoelekea kuitumikia taifa hili katika wadhifa mpya, huku tukimtakia kila la heri,” aliongeza Gachagua.