Home Habari Kuu Wanawake watakiwa kujiunga kwa vikundi ili kupata fedha za serikali

Wanawake watakiwa kujiunga kwa vikundi ili kupata fedha za serikali

Mama Taifa Rachel Ruto, amewahimiza wanawake kujiunga katika vikundi ili kunufaika na hazina za serikali.

0
Mama Taifa Rachel Ruto akutana na makundi ya wanawake katika kaunti ya Mombasa.

Mama Taifa Rachel Ruto, amewahimiza wanawake kujiunga katika vikundi ili kunufaika na hazina za serikali pamoja na taasisi zingine za fedha, kama vile mpango wa table banking.

Mama taifa aliyasema hapo wakati wa mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi katika eneo la Mikindani, kaunti ya Mombasa ambao uliwaleta pamoja wanawake kutoka maeneo bunge ya Jomvu, Mvita, Likoni, na Changamwe.

Kwa upande wake waziri wa jinsia, utamaduni, sanaa na turathi Aisha Jumwa ambaye pia alihudhuria mkutano huo, alisema serikali imetenga shilingi milioni 946 ambazo zitapatikana kupitia hazina ya kuwawezesha wanwake ambayo inapatikana kidijitali kupitia  *254#.

Jumwa alisema upatikanaji wa hazina hiyo kupitia mfumo wa kidijitali wa *254#, unawaondolea wanawake changamoto wanakumbana nazo wanapotuma maombi ya kupata fedha hizo.

Mwakilishi wanawake kaunti ya Mombasa Zamzam Mohammed, alitoa wito kwa Rais kuongeza fedha katika hazina hiyo, ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka miongoni mwa wanawake.

Website | + posts