Home Habari Kuu Wanasiasa wawili wazuiliwa kabla ya maandamano Uganda

Wanasiasa wawili wazuiliwa kabla ya maandamano Uganda

0
kra

Vikosi vya usalama vya Uganda vimezingira nyumba za wanasiasa mashuhuri wa upinzani, kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu, Kampala.

Kiongozi mkongwe wa upinzani Kizza Besigye na Bobi Wine, mwimbaji nyota wa zamani ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, wanasema kuwa vikosi vya usalama vinazingira nyumba zao na kuwazuia kuondoka.

kra

“Wanajeshi waoga na polisi wamezingira nyumba yetu na kutuweka chini ya kizuizi cha nyumbani, lakini maandamano yanaendelea,” Bw Kyagulanyi alisema katika mtandao wa X.

Besigye pia alishiriki chapisho muda mfupi baadaye, huku picha zikionyesha maafisa kadhaa wa usalama wakizuia lango la kuingia nyumbani kwake.

“Tumezuiliwa nyumbani na waoga! Hakuna kurudi nyuma; tunastahili bora,” alinukuu picha hizo.

Wakosoaji hao wawili wa serikali wamewataka Waganda kuendelea na maandamano yaliyopangwa siku ya Alhamisi ya kuitaka serikali kurekebisha barabara zilizochakaa.

Polisi wameapa kuzuia maandamano hayo, wakisema kuwa maandamano yaliyoandaliwa na wanasiasa “hayajawahi kuwa ya amani” na yatavuruga mkutano mkuu unaoendelea katika mji mkuu.

Baadhi ya wajumbe 4,000 wanahudhuria mkutano wa 19 wa Jumuiya ya nchi zisizofungamana na Siasa mjini Kampala.

Website | + posts
BBC
+ posts