Home Michezo Wanariadha wa Kenya warejea baada ya kutwaa taji ya chipukizi Afrika...

Wanariadha wa Kenya warejea baada ya kutwaa taji ya chipukizi Afrika mashariki

0

Timu za Kenya za riadha kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 18 na chini ya umri wa miaka 20, zimewasili nchini Jumapili alasiri kutoka visiwani Zanzibar zilipotwaa ubingwa wa jumla katika mashindano ya riadha ya Afrika mashariki.

Timu hizo zimenyakua ubingwa kwa jumla ya medali 23,dhahabu 12,fedha 6 na shaba 5 kwenye mashindano hayo yaliyoandaliwa katika uwanja wa New Amaan Complex, nchini Zanzibar baina ya tarehe 26 na 27 mwezi huu.

Washindi wa dhahabu za walikuwa:Carolyne Anyango katika urushaji sagai,Esther Atsanga na Brian Okoth katika 100m,James Gechuki na Nancy Chepng’etich mita 800,Samuel Toili,Evans Kiprono na Nancy Chepng’etich katika mita 400,Beatrice Machoka na Daniel Wasike katika mita 200 na dhahabu katika mita 400 kupokezana virojo kwa wavulana na wasichana .

Nishani za fedha zilitwaliwa na:-Rita Mwende na Beatrice Machoka katika mita 400,Evans Kiprono katika mita 200,Judith Chemutai mita 1500 na Rita Mwende mita 800.

Walionyakua medali za shaba ni pamoja na :-Daniel Kioko,Elykan Edwin katika mita 1500,Brigit Nyatichi mita na Elykanah Edwin 3000,Daniel Wasike mita 400 na Carolyne Anyango katika urushaji tufe.

Website | + posts