Home Michezo Wanariadha wa Kenya kujitosa Brussels kuwinda kitita na tiketi ya Dunia

Wanariadha wa Kenya kujitosa Brussels kuwinda kitita na tiketi ya Dunia

0
Mary Moraa akishind mbio za mita 800 katika mashindano ya Lausane Diamond League
kra

Wanariadha wa Kenya watajitosa uwanjani Ijumaa  na Jumamosi  usiku mjini Brussels katika mkondo wa mwisho wa mashindano ya Diamond League nchini Ubelgiji, wakiwania donge nono la pesa na tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao.

Mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki  Ronald Kwemoi,Cornelius Kemboi,Nicholas Kipkorir na Jacob Krop watashiriki fainali ya mita 5,000 Ijumaa usiku,wakikabiliana na Wahabeshi Yomif Kejelcha,Berihu Aregawi,Hagos Gebrehiwet na Haile Bekele.

kra

Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Abraham Kibiwott atajitosa katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji pamoja na mshindi wa nishani ya fedha ya Afrika Amos Serem na Wilberforce Kones, wakimenyana na bingwa wa Olimpiki na Dunia Soufiane El Bakkali wa Morocco na wapinzani wa kutoka Uhabeshi.

Katika mbio za mita 1,500 Boaz Kiprugut,Timothy cheruiyot,Reynold Cheruiyot na Brian Komen watashindana na bingwa wa Olimpiki Cole Hocker wa Marekani ,bingwa wa Dunia Jakub Ingebristen wa Norway na Yared Nuguse wa Marekani.

Bingwa wa Dunia na mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Mary Moraa, atakuwa Mkenya pekee kwa wanawake  atakayeshiriki mashindano usiku huu akitimka mita 800.

Fainali nyingine ya kusisimua Ijumaa usiku ni mita 100 wanawake bingwa wa Olimpiki Julien Alfred wa kisiwa cha Saint Lucia, akizindua uhasama na bingwa wa Dunia Sha Carri Richardson wa Marekani.

Fainali zaidi zitaandaliwa kesho huku mabingwa 32 kutoka kila fani wakituzwa shilingi milioni 3.9, na tiketi ya kushiriki mashindano ya Dunia Septemba mwaka ujao.

 

Website | + posts