Home Michezo Wanariadha 51 wachaguliwa kwa Michezo ya Afrika nchini Ghana

Wanariadha 51 wachaguliwa kwa Michezo ya Afrika nchini Ghana

0

Wanariadha 51 walichaguliwa kuiwakilisha Kenya katika makala ya 13 ya Michezo ya Afrika itakayoandaliwa mjini Accra, Ghana kati ya tarehe 18 na 23 mwezi huu.

Wanariadha hao ambao wataripoti kambini kwa matayarisho, walichaguliwa kufuatia majaribio ya siku mbili yaliyoandaliwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Punde baada ya uteuzi, kikosi hicho kilikabidhiwa kwa baraza la michezo nchini linalojukumika kwa kuandaa timu za Kenya zinazoshiriki michezo ya Afrika.

Idadi ya washiriki ililazimika kuongezwa kutoka 30 wa awali kufuatia mgomo ulioitishwa na wanariadha wakisusia majaribio.

Baadhi ya waliojumuishwa kikosini ni bingwa wa zamani katika urushaji wa sagai Juliua Yego, mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mita elfu tatu kuruka viunzi  na maji Beatrice Chepkoech akishiriki mita 5,000, na bingwa wa dunia katika mita 800 Mary Moraa atakayeshiriki mita 400.

Website | + posts