Home Michezo Wanariadha 30 wateuliwa kuwakilisha Kenya kwa mbio za nyika Afrika

Wanariadha 30 wateuliwa kuwakilisha Kenya kwa mbio za nyika Afrika

Timu hiyo inatarajiwa kuripoti kambini Jumapili ya Februari 11 eneo la Ngong huku naibu Rais wa chama cha riadha Kenya Paul Mutwii akiongoza kikosi hicho.

0

Wanariadha 30 wameteuliwa kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya mbio za nyika barani Afrika yatakayoandaliwa mjini Hammamet nchini Tunisia.

Kikosi kilichotajwa kinawajumuisha wanariadha chipukizi na waliobobea wengi wao wakiwa wale walioshiriki mbio za nyika za Sirikwa Classic wiki jana mjini Eldoret.

Kikosi cha kilomita 6 wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 kitaongozwa na mshindi wa mshindi wa nishani ya fedha ya katika mbio za Sirikwa Diana Chepkemoi, huku timu ya kilomita 10 wasichana ikiongozwa na Winfred Mbithe na Sandrafelis Chebet.

Titus Kiprotich ataongoza kikosi cha kilomita 8 wavulana chini ya umri wa miaka 20 wakati Vincent Langat akijumuishwa katika timu ya kilomita 10 wanaume.

Veronicah Mbithe awaongoza wanariadha wa mbio za kupokezana kijiti

Timu hiyo inatarajiwa kuripoti kambini Jumapili ya Februari 11 eneo la Ngong huku naibu Rais wa chama cha riadha Kenya Paul Mutwii akiongoza kikosi hicho.

Kikosi kamili kilichoteuliwa kinawajumuisha:-

Kilomita 6 wasichana

1.Diana Chepkemoi

2.Sheila Jebet

3.Judy Kemunto

4.Nancy Cherop

5.Lucy Wambui

6.Sharon Chepkemoi

Kilomita 8 wavulana

1.Titus Kiprotich

2.Gideon Kingetich

3.Clinton Kimutai

4.Simon Maywa

5.Joash Ruto

6.Joseph Wanjiru

Kilomita 10 wanawake

1.Cinthia Chepngeno

2.Grace Loibach

3.Virginia Nyambura

4.Caren Chebet

5.Gladys Mong’are

6.Sandrafellis Chebet

Kilomita 10 wanaume

1.Naibei Kiplimo

2.Vincent Langat

3.Fredrick Domongole

4.Robert Koech

5.Brian Kiptoo

6.Vincent Kimaiyo

Mbio za kupokezana

1.Mirriam Cherop

2.Evaline Chepkoech

3.Winfred Mbithe

4.Edwin Kiprono

5.Victor Mutai

6.Newton Cheruiyot

Website | + posts