Home Habari Kuu Wanapatholojia wakamilisha awamu ya tatu ya ukaguzi wa miili Shakahola

Wanapatholojia wakamilisha awamu ya tatu ya ukaguzi wa miili Shakahola

0

Kundi la wanapatholojia na majasusi limekamilisha awamu ya tatu ya uchunguzi wa miili ambayo ilifukuliwa kutoka msitu wa Shakahola inayoaminika kuwa ya wafuasi wa mhubiri tata Paul Mackenzie.

Likiongozwa na mpasuaji mkuu wa serikali Daktari Johansen Oduor, kundi hilo limesema kwamba kufikia sasa, limekagua miili 338 kwenye awamu zote, tangu mwanzo wa mchakato huo.

Uchunguzi wa mwili wa mfuasi mmoja wa Mackenzie ambaye alifariki akiwa kizuizini bado haujafanywa.

Kundi hilo limeelezea kwamba litafanya ukaguzi wa mwili wa aliyefariki akiwa kizuizini pindi tu watu wa familia yake watakapowasili na kuutambua.

Leo Jumanne, wakaguzi hao walisema walishughulikia miili minane, saba ya watu wazima na mmoja wa mtoto. Mitatu ilikuwa ya wanaume huku mitano ikiwa ya jinsia ya kike. Waliongeza kwamba miili miwili haikuwa imeoza sana lakini sita ilikuwa imeoza sana.

Mmoja kati ya miili ambayo haikuwa imeharibika sana ulipatikana kuwa na majeraha kwenye kichwa huku mitatu ikionyesha dalili za kukosa chakula kwa muda mrefu.

Walishindwa kubaini chanzo cha vifo vya watu watatu ambao miili yao ilikaguliwa leo kwa sababu ilikuwa imeharibika sana.

Kulingana na wakaguzi hao, awamu nyingine ya ufukuzi itaanza wakati wowote kutoka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here