Home Biashara Wanaouza miraa ughaibuni wateta uamuzi wa kufurushwa JKIA

Wanaouza miraa ughaibuni wateta uamuzi wa kufurushwa JKIA

0

Wauzaji wa miraa nje ya nchi wamelalama kufuatia uamuzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini, KAA kuwafurusha kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKIA.

Kwa mujibu wa arifa ya KAA, wenye mizigo yote ya miraa na maparachichi kuanzia Oktoba 9 watakuwa wakipakia na kuhifadhi mizigo yao katika  mabohari ya kibinafsi  yaliyo nje ya uwanja wa ndege wa JKIA.

Chama cha wafanyabiashara wa Nyambene kimesema kuwa uamuzi huo uliafikiwa bila kuhusishwa kwao kwa kutumia porojo.

KAA inayoongozwa na kaimu Meneja Mkurugenzi Henry Ogoye imesema kuwa iliafikia uamuzi huo kutokana na wafanyabiashara wa miraa ambao wamekuwa wakirandaranda, kusongamana na kutupa taka ovyo katika uwanja wa JKIA kuwa sababu kuu ya kuwatimua kutokana uwanja huo.

Wafanyabiasha hao wanataka muda zaidi kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo ambalo wanahisi litaathiri usafirishaji wa miraa kutoka Kenya hadi Somalia, Siera Leone na Israel.

Website | + posts