Home Habari Kuu Wanaoishi kwa nyumba za serikali walalamikia ilani ya kuhama

Wanaoishi kwa nyumba za serikali walalamikia ilani ya kuhama

0

Wafanyikazi wanaoishi kwa nyumba za serikali mtaani Jogoo Road wanalalama hatua ya serikali kuwaamrisha kuhama mara moja ,ili kupisha ubomozi na ujenzi wa nyumba za gharama ya bei nafuu.

Kulingana na arifa iliyoandikwa Februari 27 na katibu katika wizara ya nyumba na mijengo ya mjini Charles Hinga, nyumba zitakazobomolewa ni za mitaa ya Mbotela,Jogoo Road Phase 1 na 2,Jamaa,Ahero na Mawenzi Gardens.

Zaidi ya wanyakizaki 1,000 wa serikali wanatarajiwa kuathirika huku wengi wakilipa kodi ya shilingi 4,500 kwa mwezi kwa chumba cha chumba kimoja cha kulala na shilingi 7,500 kwa chumba chenye vyumba viwili vya kulala.

Wapangaji hao wanataka wapewe muda zaidi ili kujipanga kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo.

Kulingana na Hinga ubomoaji wa nyumba hizo utaanza April mwaka hu.

Website | + posts