Home Habari Kuu Wanaoeneza chuki kaunti ya Lamu waonywa

Wanaoeneza chuki kaunti ya Lamu waonywa

Waziri Kindiki aliyasema hayo Alhamisi asubuhi baada ya kukadiria hali ya usalama katika eneo bunge la Lamu Magharibi, kaunti ya Lamu.

0

Waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure Kindiki ameagiza kufanywa uchunguzi ili kuwatia nguvuni na kuwafungulia mashtaka watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuchochea chuki za kidini na kikabila katika kaunti ya Lamu.

Agizo hilo lilijiri baada ya kusambazwa kwa video iliyowaonyesha baadhi ya viongozi wakidai kuwa wanabuni vuguvugu la kuwafurusha baadhi ya jamii katika kaunti ya Lamu.

“Msako umeanzishwa na wahusika wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza chuki za kidini na kikabila watakamatwa na kufunguliwa mashtaka,” alisema Waziri Kindiki.

Waziri Kindiki aliyasema hayo Alhamisi asubuhi baada ya kukadiria hali ya usalama katika eneo bunge la Lamu Magharibi, kaunti ya Lamu.

Alisema serikali imehakikisha hali ya usalama inapewa kipaumbele katika kaunti hiyo ili kutokomeza magaidi, wahalifu na wanaoeneza itikadi kali.

Akipongeza hatua ambazo zimepigwa na asasi za usalama katika operesheni ya Linda Boni, aliwaaifu maafisa wa usalama kwa kujitoa mhanga na Kwa uzalendo wao.

Website | + posts