Home Kimataifa Wanaodharau jeshi kupokonywa mali yao nchini Urusi

Wanaodharau jeshi kupokonywa mali yao nchini Urusi

0

Wabunge wa bunge la chini, nchini Urusi linalofahamika kama “State Duma” wamepitisha sheria inayodhamiriwa kudhibiti watu ambao wanadharau jeshi.

Itakapotiwa saini na kuanza kutumika sheria hiyo itasababisha watu ambao watapatikana na hatia ya kudharau jeshi wanyanganywe mali yao.

Mswada huo sasa unaelekezwa katika bunge la juu nchini Urusi kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa au kukataliwa.

Hatua ya mwisho itakuwa ya Rais Vladmir Putin kuutia saini kuwa sheria.

Spika wa bunge hilo la chini Vyacheslav Volodin alisema kwamba mswada huo unalenga kudhibiti wasaliti wasiotambua juhudi za wanajeshi wa Urusi, wanaosaliti nchi yao na wanaofadhili wanajeshi wa nchi inayozozana na Urusi.

Tayari dharau kwa jeshi la Urusi ni hatia chini ya sheria ya mwaka 2022 iliyopitishwa kwa lengo la kudhibiti wapinzani wa hatua ya Urusi ya kuvamia Ukraine.

Sheria hiyo inahusisha makosa kama vile kuhalalisha ugaidi na kusambaza habari za uwongo kuhusu jeshi na imetumiwa sana kunyamazisha wakosoaji wa Rais Putin.

Wanaharakati, wanablogu na raia wengine wa Urusi wamehukumiwa vifungo virefu gerezani au kutozwa faini kwa kulaani vita hivyo.

Website | + posts