Shirikisho la soka duniani FIFA, limetangaza orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka huu kwa wanaume na wanawake .
Wanaowania tuzo ya wanaume ni; Kylian Mbappe wa Paris St Germain na Ufaransa,Lionel Messi wa Argentina na aliichezea timu ya Paris St Germain, kabla ya kuhamia Inter Miami na Erling Haaland wa Norway na Manchester City.
Katika tuzo ya wanawake wanandinga watatu wa mwisho walioteuliwa ni; Aitana Bonmatí wa Uhisapani na klabu ya FC Barcelona,Linda Caicedo wa Colombia na klabu ya Deportivo Cali Femenino na Real Madrid,Jennifer Hermoso wa Uhispania na klabu ya Pachuca Femenil.
Wachezaji hao waliteuliwa kwa kuzingatia matokeo ya baina ya Agosti mwaka 2022, hadi Agosti 20 mwaka huu.
Wanahabari, Makocha na Manahodha wa timu za taifa wanachama wa FIFA hupiga kura kubaini washindi wa tuzo hizo.
Washindi watanainika Januari 15 mwaka ujao jijini London Uingereza.