Home Habari Kuu Wanamgambo wawili wa Al Shabaab wauawa Lamu

Wanamgambo wawili wa Al Shabaab wauawa Lamu

Kaunti ya Lamu imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al shabaab wanaovuka mpaka kutoka Somalia na kuingia nchini.

0

Wanamgambo wawili wa kundi la Al Shabaab waliuwa Jumamosi kufuatia makabiliano makali dhidi ya wanajeshi katika eneo la Bodhei kaunti ya Lamu .

Kulingana na taarifa kutoka kwa maafisa wa usalama ,wanajeshi hao walipata bunduki tatu aina ya AK47 na zaidi ya risasi 300 na silaha nyinginezo.

Wanamgambo hao walikuwa wamejificha katika msitu wa Boni Forest na walipatikana wakati wanajeshi waliendesha oparesheni kubaini maficho yao mawili.

Yamkini walikuwa wanapanga kutekeleza shambulizi eneo la Lamu.

Kaunti ya Lamu imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al shabaab wanaovuka mpaka kutoka Somalia na kuingia nchini.

Website | + posts