Home Habari Kuu Wanajeshi wa Kenya warejea kutoka DRC

Wanajeshi wa Kenya warejea kutoka DRC

0

Wanajeshi wa Kenya waliokuwa wakilinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wamerejea nchini leo Alhamisi.

Kundi la pili la wanajeshi hao limepokelewa katika kambi ya jeshi ya Embakasi na Mkuu wa Majeshi Jenerali Francis Ogola.

Wanajeshi wa Kenya walikuwa wakihudumu katika kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichokuwa kikishika doria nchini DRC.

Hata hivyo, wanajeshi hao wamelazimika kurejea baada ya DRC kukataa kuongeza muda wa kuhudumu.