Home Habari Kuu Wanajeshi kuchunguza chanzo cha kifo cha Mkuu wa majeshi Jenerali Ogolla

Wanajeshi kuchunguza chanzo cha kifo cha Mkuu wa majeshi Jenerali Ogolla

0

Ndege ya Kijeshi na maafisa kadhaa imepelekwa katika eneo la ajali ya ndege ya siku ya Alhamisi eneo la Marakwakwet Mashariki, kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo iliyosabibisha kifo cha Mkuu wa Majeshi Jenerali Ogolla na maafisa wengine tisa.

Kwenye hotuba yake kwa taifa kutoka ikulu Rais William Ruto alielezea masikitiko yake kufuatia kifo cha Jenerali Ogolla, ambaye ni Mkuu wa majeshi wa kwanza kufariki akiwa afisini katika historia ya Kenya.

Marehemu Ogolla aliye na umri wa miaka 61 alikuwa akiongoza misheni ya kurejesha amani eneo la Pokot Magharibi linalokabiliwa na changamoto ya wizi wa mifugo na kuandaa shule ili wanafunzi warejee punde muhula mpya utakaanza mwezi ujao.