Home Habari Kuu Wanajeshi kadhaa wauawa Lamu na Al-Shabaab

Wanajeshi kadhaa wauawa Lamu na Al-Shabaab

Yamkini idadi isiyojulikana ya wanajeshi wameaua,kejeruhiwa vibaya katika shambuliz hilo.

0

Wanajeshi kadhaa  wanahofiwa kufariki  jana Jumapili usiku, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga  vilipuzi katika msitu wa Boni kaunti ya Lamu, kwenye shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na kundi  la Al-Shabaab.

Yamkini idadi isiyojulikana ya wanajeshi wameuawa na kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo.

Msemaji wa wanajeshi Brigadia  Ziporah Kioko mapema leo Jumatatu amethibitisha kuwa  gari hilo lilipuliwa kwa bomu lililokuwa limetegwa barabarani na Al-Shabaab, wanajeshi wakiwa katika zamu ya kushika doria katika barabara ya Bodhei-Majengo.

Wanajeshi wamewaomba raia kutoa taarifa kuhusiana na visa vyovyote wanavyoshuku kuwa vya Al-Shabaab.

Website | + posts