Home Kaunti Wanaharakati wapongeza mahakama kwa kuharakisha kesi ya mauaji ya mwenzao

Wanaharakati wapongeza mahakama kwa kuharakisha kesi ya mauaji ya mwenzao

0
kra

Watetezi wa haki za binadamu wameridhika na hatua ya idara ya mahakama kushughulikia haraka kesi ya mauaji ya mwanaharakati mwenzao kwa jina Elizabeth Ibrahim Ekaru.

Grace Lolen mmoja wa wanaharakati hao aliyezungumza baada ya kuhudhuria kikao cha kesi hiyo katika mahakama kuu ya Meru, aliishuruku mahakama kwa kushughulikia kesi hiyo haraka.

kra

Grace mkazi wa kaunti ya Isiolo amewataka watu hasa wanawake wanaodhulumiwa kujitokeza na kupaaza sauti badala ya kutumia mbinu za kinyumbani za kutatua kesi za dhuluma dhidi ya wanawake.

Marehemu Elizabeth Ibrahim Ekaru alikuwa mtetezi wa haki za wanawake, haki za umiliki wa ardhi na alikuwa akihimiza amani na utunzi wa mazingira katika kaunti ya Isiolo.

Wakili Zaina Kombo ambaye hushughulikia kesi za haki za binadamu alipongeza mahakama, wananchi na vyombo vya habari kwa usaidizi wa kuhakikisha haki inatendeka kwa kesi hiyo ya Elizabeth.

Jaji wa mahakama kuu ya Meru Edward Muriithi ameweka Julai 25, 2025 kuwa tarehe ya kuamua kesi hiyo.

Elizabeth alitambulika kwa kazi zake kiasi cha kupatiwa tuzo ya “Head of State Commendation”.

Alikuwa Jumatatu Januari 3, 2022 na Patrick Naweet mshukiwa mkuu wa kesi hiyo kutokana na ugomvi kuhusu ardhi.

Mama huyo wa watoto watano alidungwa kisu katika eneo la Kambi Garba kaunti ya Isiolo wakati alikuwa akihudhuria mazishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here