Home Kaunti Wanaharakati wa kupambana na ukeketaji waanzisha kampeni huko Pokot Magharibi

Wanaharakati wa kupambana na ukeketaji waanzisha kampeni huko Pokot Magharibi

0

Wanaharakati wa kupambana na ukeketaji wameanzisha kampeni ya kupambana na ukeketaji katika kaunti ya Pokot Magharibi wameungana kuanzisha kampeni dhidi ya uovu huo ambao umesababisha wasichana wengi kuacha shule na kuingia kwenye ndoa za mapema.

Makundi mbali mbali ya uanaharakati katika kaunti hiyo yameapa kushirikiana kupambana na uovu huo ili kuhakikisha wasichana wanafahamu hatari na athari zake ili kuepuka kudanganywa na wakeketaji kisiri.

wahasiriwa wa ukeketaji wanaishi kwa hofu katika kaunti hiyo na wanaogopa kuwasema wanaokeketa wanao ambao wakati mwingine ni wanafamilia na woga huo umesababisha wasichana wengi zaidi kukeketwa kisiri.

Mercy Tumkuo kutoka kundi moja linalohamasisha kuhusu athari za ukeketaji anasema wameanzisha kampeni kabambe mashinani watoto wapelekwe shule ndiposa wasipatikane nyumbani na kufanyiwa uovu huo.

Wakati wa kampeni katika eneo la Nakuyen kwenye mpaka wa Kenya na Uganda wadau waliwasihi wazazi kuelekeza wanao wanapokua kwa kuwapa mazingira salama.

Mwanaharakati mwingine kwa jina Everlyne Prech naye anasema watoto wanastahili kulindwa kutokana na maovu yote na wazazi wa maeneo ya mashinani wanafaa kusaidiwa kufahamu jinsi ya kutunza wanao na kuhakikisha hawalazimishwi kukeketwa au kuingia kwenye ndoa za mapema.

Masika Mwigi kutoka DSTW alisema lengo la kuungana kwao ni kutetea mtoto msichana katika kaunti ya Pokot Magharibi aliye katika hatari ya kukeketwa.

Watasaidia pia wahasiriwa wa ukeketaji ambao wanaendelea kupona kutokana na kiwewe cha ukeketaji.

Kulingana na Masika wanaharakati katika mashirika yao mbali mbali wanashirikiana na serikali kuu na ile ya kaunti kupambana na ukeketaji.

Mercy Cheruto afisa wa utunzaji wa watoto katika shirika la World Vision alisema wanatumai sheria itatekelezwa mashinani ili kupambana na ukeketaji.

Website | + posts