Home Vipindi Wanaharakati wa haki za binadamu wapongeza marufuku ya Muguka Kilifi

Wanaharakati wa haki za binadamu wapongeza marufuku ya Muguka Kilifi

kra

Wanaharakati wa haki za binadamu katika kaunti ya Kilifi wamempongeza Gavana Gideon Mung’aro kwa kupiga marufuku mauzo na matumizi ya Muguka katika kaunti hiyo wakisema ni hatua bora ya kukabiliana na tatizo la uraibu wake.

Wanasema Muguka unaharibu watoto wadogo na wakamhakikishia Gavana Mung’aro kwamba watamuunga mkono hadi agizo lake litakapotekelezwa kikamilifu.

kra

Gavana Mung’aro alipiga marufuku mmea huo wa Muguka Ijumaa kupitia amri yake na akawa Gavana wa pili kufanya hivyo katika eneo la Pwani baada ya mwenzake wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir.

Awali wanaharakati hao waliomwomba Gavana Mung’aro kupiga marufuku Muguka na ujio wa amri hiyo ni furaha kwao kwani wanahisi ombi lao lilijibiwa.

Wakizungumza huko Malindi wanaharakati hao walisema kwamba mmea huo unafaa kupigwa marufuku katika eneo zima la Pwani.

Victor Kaudo mmoja wa wanaharakati hao alihimiza magavana wa kaunti za Kwale, Lamu, Tana River na Taita Taveta kufuata nyayo za wenzao wa Mombasa na Kwale.

Kaudo aliyekuwa akizungumza katika eneo la Maono Hub huko Malindi alisema hatua hiyo ilikuwa imechelewa kwani Muguka unasababisha madhara makubwa kwa wanaotumia.

Wanaharakati Jacinta Mbeyu na Fatuma Mohamed walikariri maoni sawa na hayo.

Website | + posts
Dickson Wekesa
+ posts