Home Kaunti Wanafunzi wa shule za msingi Bungoma wapokea visodo

Wanafunzi wa shule za msingi Bungoma wapokea visodo

Mbunge Jack Wamboka alisema kuwa ukosefu wa visodo kwa wanafunzi wa kike wakati wa hedhi, umeathiri matokeo yao shuleni kwa sababu wanakosa kuhudhuria masomo.

0
Wanafunzi wapokea Visodo kaunti ya Bungoma.

Wanafunzi kutoka shule saba za msingi eneobunge la Bumula, kaunti ya Bungoma, wamepokea visodo kutoka kwa mbunge wa eneo hilo Jack Wamboka.

Kupitia mpango wa Wamboka Wanami, wanafunzi wa kike walipokea visodo hivyo ili kuwapa fursa ya kuhudhuria masomo bila kukosa wakati wa hedhi na pia kulinda afya yao.

Mbunge huyo alisema kuwa ukosefu wa visodo kwa wanafunzi wa kike wakati wa hedhi, umeathiri matokeo yao shuleni kwa sababu wanakosa kuhudhuria masomo kwa fedheha ambayo hushusha thamani yao.

Alisema kuwa kupitia mpango huo, wavulana katika shule za eneobunge hilo watapokea ushauri nasaha ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto za maisha.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Lunao, Wamboka aliwaomba wazazi na jamii kwa jumla kuepukana na hulka ya kutatua kesi za ubakaji nje ya mahakama akisema kuwa hiyo ni njia ya kuunga mkono uovu huo ambao umeadhiri maisha ya wasichana.

Alionya kuwa wale ambao wanatekeleza uovu huo lazima wachukuliwe hatua ya kisheria ili maovu kama hayo yakomeshwe katika jamii.

Alphas Lagat
+ posts