Home Biashara Wanafunzi 20 wahitimu kutoka kituo cha MTF

Wanafunzi 20 wahitimu kutoka kituo cha MTF

0

Wanafunzi 20 jana Alhamisi walihitimu katika taaluma ya utengenezaji filamu kutoka kituo cha Multi-Choice Talent Academy (MTF) jijini Nairobi.

Wanafunzi hao 20 kutoka mataifa manne ya Ethiopia, Tanzania, Uganda na Kenya wamekuwa wakipokea mafunzo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kituo cha MTF kiliasisiwa mwaka 2018 kwa lengo la kukuza vipaji vya ubunifu katika sekta ya filamu Afrika.

‚ÄúTumejizatiti kuendelea kuelezea hadithi za bara Afrika na hususan Afrika Mashariki kwa njia za kisasa zinazoambatana na mabadiliko ya uhalisia wa maisha,” alisema Victoria Goro ambaye ni Mkurugenzi wa MTF Academy Afrika Mashariki.

Mkurugenzi wa Multi-Choice Kenya, Nzola Miranda amesema kituo hicho kinatekeleza wajibu muhimu kuendeleza tasnia ya filamu.

“Mwaka huu, tutahakikisha wanafunzi waliohitimu leo wanapata nasafi za mafunzo ya nyanjani na hata kazi katika baadhi ya kampuni washirika wetu,” alisema Miranda.

Mkurugenzi wa Multi-Choice Nzola Miranda akimkabidhi tuzo mmoja wa mahafali

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba aliahidi kuwa serikali itaendeleakulea na kukuza talanta za wasanii nchini.

Kituo cha MTF tayari kimetoa mafunzo kwa zaidi ya wanafunzi 300 tangu kubuniwa kwake.

Website | + posts