Takriban wanafunzi 16 wameripotiwa kufariki baada ya moto kuteketeza moja ya mabweni katika shule ya Hillside Endarasha katika Kaunti ya Nyeri.
Vyanzo vya habari vinaonyesha kuwa wanafunzi walioaga dunia walichomwa kiasi cha kutoweza kutambulika katika moto huo wa Alhamisi usiku.
Wanafunzi wengine kumi na wanne wamekimbizwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya ya moto. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Kufuatia hili, maafisa wakuu wa polisi wako njiani kuelekea katika shule hiyo.
Tutakuletea habari zaidi baadaye.