Home Kimataifa Wanafunzi 144,102 watuma maombi ya kujiunga na elimu ya juu kupitia KUCCPS

Wanafunzi 144,102 watuma maombi ya kujiunga na elimu ya juu kupitia KUCCPS

Usajili huo ni wa juu zaidi kuwahi kunakiliwa tangu kuanza kwa zoezi hilo February 7 mwaka huu.

0
kra

Wanafunzi 22,307 waliofanya mtihani wa KCSE mwaka 2023, wametuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu pamoja na vyuo vingine kupitia mtandao wa huduma za kuwasajili wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo KUCCPS, katika muda wa saa 24 zilizopita.

Ufanisi huo umetokana na kubuniwa kwa kamati ya pamoja ya maafisa wa KUCCPS na eCitizen, ambao walijizatiti kutatua changamoto zilizodumaza usajili wa wanafunzi hao hapo awali.

kra

Usajili huo ni wa juu zaidi kuwahi kunakiliwa tangu kuanza kwa zoezi hilo February 7 mwaka huu.

Kufikia tarehe moja mwezi Machi, wanafunzi 144,102, hii ikiwa ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 199,695 waliopata alama ya C+ na zaidi katika mtihani wa KCSE mwaka 2023, walikuwa wametuma maombi ya kujiunga na vyuo vikuu na vyuo.

KUCCPS inatarajia kuwa wanafunzi 173,178 hii ikiwa ni asilimia 86 ya wanafunzi waliopata alama ya C+ na zaidi watatuma maombi hayo.

Aidha wanafunzi ambao bado hawajatuma maombi yao, wametakiwa kufanya hivyo kabla ya kukamilika kwa zoezi hilo Jumatatu Machi, 4 , 2024.

Website | + posts