Home Kimataifa Wanafunzi wasiopungua 10 wa Chuo Kikuu cha Kenyatta wafariki katika ajali

Wanafunzi wasiopungua 10 wa Chuo Kikuu cha Kenyatta wafariki katika ajali

Basi hilo lilikuwa na abiria 58, waliokuwa wakielekea Mombasa kwa ziara ya kimasomo.

0

Wanafunzi wasiopungua 10 wa Chuo Kikuu cha Kenyatta wameripotiwa kufariki katika ajali ya barabarani leo Jumatatu jioni.

Hii ni baada ya basi la chuo hicho kugongana na lori lililokuwa likielekea Nairobi katika eneo la Maungu, Voi katika kaunti ya Taita Taveta.

Basi hilo lililokuwa likielekea Mombasa wakati wa ajali hiyo lilikuwa na wanafunzi 58 waliokuwa wakielekea kwa ziara ya kimasomo.

Majeruhi wengine walikimbizwa katika hospitali mbalimbali kupokea matibabu.

Hata hivyo, maelezo ya kina kuhusiana na ajali hiyo bado hayajatolewa kwani hadi kufikia sasa, mamlaka bado hazijatoa taarifa rasmii kuihusu.

Tutakuarifu zaidi kuhusiana na ajali hiyo punde baada ya maelezo ya kina kutolewa.

Ajali hiyo inatokea siku moja baada ya basi la shule ya upili ya Kapsabet kuanguka na kusababisha vifo vya mwalimu mmoja na mwanafunzi mmoja.

Wanafunzi wengine kadhaa walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo iliyotokea kwenye barabara ya Kabarnet-Marigat katika kaunti ya Baringo.

Kumekuwa na idadi inayoongezeka ya ajali za barabarani na kusababisha miito kutolewa kwa serikali kuingilia kati na kuhakikisha utiifu wa sheria za barabarani.

Website | + posts