Idadi ya watu waliofariki kwenye mkasa wa mlipuko wa lori la mafuta hapo jana nchini Nigeria imepanda hadi 48.
Kulingana na shirika la kiserikali la kukabiliana na mikasa, lori la mafuta liligongana ana kwa ana na lori lingine lililokuwa limewabeba abiria na kusababisha mlipuko mkubwa.
Mkasa huo unajiri wakati taifa hilo linalozalisha mafuta mengi barani Afrika linakumbwa na uhaba wa bidhaa hiyo, baada ya shirika la mafuta NNPC kupandisha bei kwa asilimia 39 wiki jana.
Hatua hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa waendeshaji magari waliopiga foleni ndefu kununua bidhaa hiyo muhimu.