Home Habari Kuu Walio na ulemavu wapewe fursa sawa, asema Dorcas Rigathi

Walio na ulemavu wapewe fursa sawa, asema Dorcas Rigathi

Dorcas alisema kila mtu ana haki ya kupewa nafasi sawa katika nyanja zote za jamii.

0

Mkewe naibu rais mhubiri Dorcas Rigathi anashinikiza kubuniwa kwa sera zitakazotoa fursa sawa kwa watu walio na ulemavu.

Akiongea alipozindua rasmi hafla ya mwaka huu ya ukweaji mlima Longonot kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuona mjini Naivasha, kaunti ya Nakuru, Dorcas alisema kila mtu ana haki ya kupewa nafasi sawa katika nyanja zote za jamii.

“Tutaendelea kushinimiza kubuniwa sera ili tunapozungumza kuhusu thuluthi mbili wa kijinsia na ushawai, tunaweza pia zungumza kuhusu wao kupewa asilimia Fulani katika ajira ili wasiachwe nje,” alisema Dorcas.

Mhubiri Dorcas pia alishiriki kwenye hafla hiyo.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na chama cha watu wasiokuwa na uwezo wa kuona humu nchini, inalenga kuchangisha pesa za kununua vifaa vinavyohitajika kurahisisha masomo ya watoto wasiokuwa na uwezo wa kuona.

“Kila mmoja licha ya uwezo wake wa kuona anahitaji fursa sawa ya elimu, ajira na fursa zingine zilizopo” aliongeza Dorcas.

Akiongea katika hafla hiyo, afisa mkuu mtendaji wa chama cha watu wasiokuwa na uwezo wa kuona humu nchini, Samson Waweru alilalamikia ubaguzi unaoendelea miongoni mwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuona katika jamii.

Maslahi ya watu wenye mahitaji maalum ni mojawapo ya masuala yanayoangaziwa na afisi ya mkewe naibu rais Pastor Dorcas Rigathi.

Website | + posts