Tume ya kuwaajiri walimu, TSC imetangaza nafasi za kazi 36,275 kwa walimu watakaopandishwa vyeo.
Tangazo hili linajiri wiki moja pekee baada ya tume hiyo kutangaza kuwapandisha ngazi walimu wengine 14,000 wa viwango vya juu vya usimamizi.
Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Macharia, walimu watakaopandishwa vyeo ni wale wa nyadhfa za chini pekee.
Walimu wanaoafiki matakwa yaliyowekwa wanahitajika kutuma maombi kupitia kwa “portal” ya TSC.
Nafasi 12,716 zitakuwa za walimu wa kiwango cha gredi C4 huku nyingine 10,819 zikiwa za walimu waandamizi, kiwango cha C2 na 1,049 zikiwa nafasi za walimu wakuu.