Home Kaunti Walimu wakuu waonywa dhidi ya kuwafukuza wanafunzi

Walimu wakuu waonywa dhidi ya kuwafukuza wanafunzi

0

Mkurugenzi wa Huduma ya Ukaguzi wa Hesabu za Matumizi ya Pesa za Shule wa Wizara ya Elimu Victoria Angwenyi amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari wasiwafukuze wanafunzi walio na madeni ya karo.

Akiongea jijini Mombasa wakati wa mkutano wa kitaifa wa 46 wa walimu wakuu wa shule za sekondari, Angwenyi alisema shule hutegemea wafadhili wawili wakuu ambao ni mgao wa serikali na karo zinazolipwa na wazazi.

Pia aliwataka walimu wakuu kutoa mwongozo kwa wazazi kuhusu kujiunga na shule za malazi na za kutwa kwa watoto wao kulingana na uwezo wao wa kifedha.

Wizara ya Elimu hulipa karo ya shillingi elfu 22,244 kwa kila mwanafunzi wa shule za sekondari za umma na shillingi elfu 57,974 kwa kila mwanafunzi wa shule za sekondari za wanafunzi walio na mahitaji maalum.

Angwenyi alisema suala la kuwafukuza wanafunzi halipaswi kuwepo kwa sababu serikali imetenga pesa za kugharimia masomo kwa shule zote za umma.

Kuhusu kuongezwa kwa karo, afisa huyo alisema serikali inatafuta njia za kuhakikisha shule zinatoza karo nafuu ili kuwapunguzia wazazi mzigo.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here