Home Biashara Wakuzaji kahawa wa Colombia wahimizwa kushirikiana na Kenya

Wakuzaji kahawa wa Colombia wahimizwa kushirikiana na Kenya

Gachagua alitoa wito kwa wanunuzi wa kahawa wa kimataifa kuzuru Kenya na kununua zao hilo moja kwa moja kutoka kwa wakulima.

0
Kongamano la wakuzaji kahawa laandaliwa nchini Colombia.

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa wakulima wa kahawa wa Colombia, kushirikiana na Kenya kwa lengo la kuboresha biashara ya kahawa hapa nchini.

Akizungumza siku ya Ijumaa Jijini Medellin nchini Colombia ambako alihudhuria kongamabo la saba la wakuzaji kahawa, naibu Rais alipigia debe Kenya kuandaa kongamano lijalo la nane kuhusu kahawa mnamo mwaka 2024.

Naibu huyo wa Rais alikuwa ameandamana na waziri wa kilimo  Mithika Linturi, katibu katika afisi ya naibu Rais Julius Korir, Gavana wa Bomet Hillary Barchok, mwenyekiti wa kamati ya kilimo katika bunge le Senate Kamau Murango, mwenyekiti wa wabunge wanaotoka maeneo yanayokuza kahawa mbunge Duncan Mathenge na mwenyekiti wa kamati ya nishati katika bunge la Senate Wahome Wamatinga

Wakati huo huo, Gachagua alitoa wito kwa wanunuzi wa kahawa wa kimataifa kuzuru Kenya na kununua zao hilo moja kwa moja kutoka kwa wakulima.

Katika mkutano huo, Gachagua alisema kahawa kutoka Kenya ndio bora zaidi duniani, lakini mkulima hafaidiki na ukuzaji wa zao hilo.