Home Habari Kuu Wakurugenzi sita wa NHIF wateuliwa ,Elijah Wachira akiwa Mkrugenzi Mkuu

Wakurugenzi sita wa NHIF wateuliwa ,Elijah Wachira akiwa Mkrugenzi Mkuu

0

Halmashauri ya bima ya kitaifa ya matibabu, NHIF imetangaza uteuzi wa Elijah Wachira kuwa Afisa Mkuu Mtendaji  na wakurugenzi wengine sita wa bodi hiyo.

Uteuzi huo ulitokana na mchakato wa wazi wa uajiri uliofanywa  kupitia kwa tangazo la mitandaoni Juni 27 mwaka huu.

Wakurugenzi kwenye bodi hiyo ni  Bi Hazel Koitaba, atakayesimamia hazina hiyo,Ibrahim Mohammed, atakayekuwa Mkurugenzi wa masuala ya mashirika,Pariken Ole Sankei ambaye ameteuliwa Mkurugenzi wa  Ukaguzi .

Catherine Mungania, atasimamia maswala ya sheria wakati Robert Ingasira, akiteuliwa Mkurugenziwa masuala ya kifedha huku Martin Ayoo akiteuliwa  Mkurugenzi wa  habari mawasiliano na Teknlojia.

Website | + posts