Home Biashara Wakulima wadogo kupata mikopo kutoka benki ya Faulu

Wakulima wadogo kupata mikopo kutoka benki ya Faulu

0

Wakulima wadogo katika sekta ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na kilimo cha mboga na matunda watapokea mikopo kutoka kwa benki ya Faulu Microfinance .

Hii inafuatia kusainiwa kwa ushirikiano baina ya benki hiyo na shirika la Ujerumani la Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) kama moja ya kuwainua wakulima wadogo katika mataifa ya Ethiopia,Uganda na Kenya.

Benki hiyo inadhamiria kutoa mikopo ya kima cha shilingi milioni 120 katika awamu ya kwanza ya majaribio kwa wakulima 400 katika kaunti sita za Kirinyaga, Meru, Muranga, Nakuru, Machakos, na Makueni ili kuwekeza katika kilimo cha unyunyuziaji mashamba maji kwa kutoa kawi ya jua,ununuzi wa mitambo ya kupoza inayotumiwa kawi ya jua na mitambo ya kukausha nafaka inayotumia kawi ya jua.

Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa benki ya Faulu Julius Ouma akiwa na kiongozi wa GIZ- EnDev Kenya Valerie Ostheimer

“Tumefurahia kusaini ushirikiano huu na GIZ kuwawezesha wajasiriamali wetu ma wakulima kote nchini.Kutokana na mradi huu tutawasaidia wakulima wadogo kumiliki mitambo inayotumia kawi ya jua kuimarisha maisha yao na kuongeza tija na pia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.”akasema Afisa mkuu mtendaji wa Faulu Bank, Julius Ouma

Wakulima katika sekta ya ufugaji ngombe wa maziwa na kilimo cha mboga na matunda wanaweza kupokeza mikopo hiyo kutoka benki ya Faulu.

“Kupitia kwa utoaji wa mikopo hiii ushiarikiano huu utawawezesha wakulima kutumia kawi ya kisasa isiyoathiri mazingira na kuongeza tija.” Akasema kiongozi wa GIZ EnDev Kenya Valerie Ostheimer

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here